Mgombea wa kiti Cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM)ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali inaenda kufanya tathimini ya Mashamba ya chai ambayo waliwapatia sekta Binafsi ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL) na kampuni ya Wakulima Tea Company (WATCO)kutokana na kushindwa mikataba ya uwekezaji ya kuongeza thamani Chai
Dkt. Samia ameyasema hayo Leo Sept 5,2025 katika uwanja wa Tandare uliopo mji mdogo wa Tukuyu wilayani Rungwe jijini Mbeya Kwenye muendelezo wa Mikutano yake ya Hadhara ya Kampeni za uchaguzi Mkuu 2025
Dkt. Samia amesema kuwa inavyoonekana kampuni hizo kazi hiyo imewashinda hivyo kinachofanyika sasa Serikali imeunda Timu ya kuyafanyia tathimini mashamba na viwanda lengo likiwa ni kuyachukua Mashama hayo pamoja na viwanda ili kuvimilikisha kwenye vyama vya Ushirika
Aidha Dkt. Samia ameyataka makampu hayo kulipa madeni ya wakulima kwani tayari walishawawekea mazingira mazuri ya uwekezaji
Leave a Reply