Baba Wa Taifa Alitufanya tuwe Wajanja, Sio Wajinga

Mgombe urais wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Salum Mwalimu amesema endapo atachaguliwa kuwa Rais atahakikisha anaanzisha viwanda vya kuchakata mazao yanayolimwa nchini hasa mkoani Arusha kunakotoka Vitunguu, na Maparachichi ili kuongeza ajira kwa Watanzania.

Amsema anashangazwa na Mazao mengi kulimwa nchini na kusafirishwa nchi jirani bila kuongezewa thamani hatua mabayo inainyima nchi fedha za kigeni huku akiongeza kuwa mataifa hayo yanawafundisha vijaa wao kutumia fursa za mataifa Jirani lakini Tanzani bado tupo nyuma. Amesema Baba wa Taifa Hayati Mwl Julius Kambarahge Nyerere hakutaka Watanznaia Wawe wajinga badala yake aliwawekea mazingira ya kujitambua, jambo ambalo bado linahitaji msukumo ili vijana wachangamkie Fursa.

Salu Mwalimu ameelza hayo wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Arusha waliojitokeza kusikiliza sera zake za kutka kuliongoza taifa la Tanzania