Rais Mwinyi azindua Soko na kituo cha Daladala,  Wananchi wamshukuru

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amefungua rasmi Soko na Kituo cha Mabasi cha Kisasa Chuini, Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Katika hotuba yake, Rais Dkt. Mwinyi ameagiza kuimarishwa kwa usafi, kuzuia biashara nje ya maeneo rasmi, kutoza kodi nafuu, na kufanya ukarabati wa mara kwa mara ili masoko yabaki katika hali nzuri.

Halikadhalika, amesisitiza uharakishwaji wa kuwaingiza wafanyabiashara sokoni na kuanza mara moja kwa huduma za kituo cha mabasi.

Aidha, amezitaka taasisi za kifedha kuwawezesha wajasiriamali kupata mikopo na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kujenga masoko ya kisasa katika maeneo mengine ikiwemo Mombasa, Kibanda Maiti na Malindi.

Soko la Chuini lina maduka 98, maghala, maegesho ya magari na vyoo 26, na limejengwa na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi.