Mgombea Urais kupitia Chama cha National League For Democracy (NLD) Mhe. Doyo Hassan Doyo amesema akifanikiwa kupata ridhaa ya Watanzania na kuwa Rais wa Nchi atahakikisha anashusha Maslahi ya wabunge wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania hadi kufikia Milioni 1.5 huku Madaktari Bingwa wakipokea Milioni 12
Doyo ameyasema hayo kwenye Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho iliyofanyika Katika Uwanja wa Stendi ya Pangani, Jijini Tanga ambapo amesema wabunge kulipwa milioni 12 ni kukosa uzalendo katika nchi ambapo wamekuwa wakitunga kanuni kwa ajili ya maisha yao
Amesema akiwa Rais, atahakikisha siku 100 za mwanzo atapiga marafuku malipo kwa Wajawazito na kutafuta vyanzo vipya vya mapato itakayosaidia kutoa huduma bora kwa Watanzania
Leave a Reply