Dkt. Mwinyi arejesha fomu ya kuogombea urais ZEC

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt Hussein Ali Mwinyi amerudisha fomu ya kugombea nafasi hiyo Tume ya Uchaguzi Zanzibar

Akiwa katika ofisi hiyo iliyopo Maisara Mjini Unguja Dkt Mwinyi amekabidhi fomu hizo kwa Mwenyekiti wa Uchaguzi Mheshimiwa Jaji George Joseph Kazi

Mara baada ya kurejesha fomu hiyo Dkt Mwinyi alizungumza na waandishi wa habari huku akiweka wazi kuwa kilichoharakisha kurejesha fomu hiyo ni urahisi wa kupata wadhamini katika mikoa yote ya unguja na Pemba

Amesema wadhamini wamekua wengi kuliko idadi ambayo imetakiwa na tumena hiyo inaonyesha imani kubwa waliyonayo dhidi yake

Zoezi la urejeshaji wa fomu kwa tume ya uchaguzi Zanzibar litatamatishwa Septemba 10, 2025