Uchaguzi Mkuu wa Tanzania Kufanyika Oktoba 29

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele, leo Julai 26, 2025 ametangaza rasmi ratiba kamili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ikiweka wazi hatua mbalimbali zitakazofuatwa kabla ya siku ya kupiga kura.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mchakato wa uchukuaji fomu za uteuzi utaanza mwezi Agosti, huku kampeni za uchaguzi zikipamba moto kwa takriban miezi miwili kabla ya Watanzania kupiga kura Tarehe 29, Oktoba 2025.

Hii hapa ndiyo Ratiba Ratiba Kamili

Agosti 9, 2025 hadi Agosti 27, 2025: Huu utakuwa muda wa kuchukua fomu za uteuzi kwa wagombea wa nafasi za Rais na Makamu wa Rais.

Agosti 14, 2025 hadi Agosti 27, 2025: kuchukua Fomu za uteuzi kugombea kiti cha Ubunge na Udiwani

Agosti 27, 2025: Hii itakuwa siku ya uteuzi wa wagombea kiti cha Rais, Makamu wa Rais, Ubunge, na Udiwani.

Agosti 28, 2025 hadi Oktoba 28, 2025: Kampeni za uchaguzi kwa upande wa Tanzania Bara

Agosti 28, 2025 hadi Oktoba 27, 2025: kampeni za uchaguzi kwa Tanzania Zanzibar, huku Oktoba 28 ikitengwa kwa ajili ya kupisha kura ya mapema.

Oktoba 29, 2025 ndiyo itakuwa Siku ya Uchaguzi Mkuu, ambapo wananchi watapiga kura kuchagua viongozi wao.