Wanaotaka kuja kuangalia uchaguzi Tanzania waombe kibali INEC

Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki Balozi Mahmoud Thabiti Kombo , amesema Tanzania wana mikataba ya makubaliano na jumuiya ya SADC pamoja na Afrika mashariki na Umoja wa Afrika katika uangalizi wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu hivyo kwa taasisi yoyote inayohitaji kuja kuangalia uchaguzi wa Tanzania waombe kibali kutoka tume ya Taifa ya uchaguzi INEC.

Balozi Kombo amesema kama Tanzania wana hiari kukubali au kukataa watu au taasisi zisizo na makubaliano na Tanzania katika suala zima la uangalizi wa uchaguzi na kuongeza kuwa kama wao hawaendi kuangalia kwao basi kama nchi pia tuna hiari ya kukataa.

Balozi Kombo ameyasema hayo Julai 23, 2025 akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa 27 wa mawaziri na maofisa waandamizi wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Aidha balozi Kombo ameongeza kuwa uchaguzi wa mwaka huu unatumia pesa za ndani kwa asilimia 100 hivyo hakuna msaada kutoka nchi yoyote ile duniani.