Wanaotumikia kifungo kisichozidi miezi 6 na Mahabusu Kupiga Kura Uchaguzi Mkuu

Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima amesema kuwa Tume imeaandaa utaratibu wa wafungwa na Maabusu kushiriki uchaguzi Mkuu 2025 Kwa kuwapa haki ya kupiga kura

Kailima ameyasema hayo Leo Julai 27,2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye Mkutano wa kati ya tume na viongozi wa vyama vya Siasa kuhusu maandalizi ya uchunguzi mkuu 2025

Kailima amesema kuwa kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo Cha 10 kwanza C na kifungu Cha 82 vya Sheria ya uchaguzi wa madiwani namba 1 mwaka 2024 kuhusiana na wafungwa wanaotumikia kifungo kisichozidi miezi 6 kuwa na sifa ya kupiga kura ambapo tume imeweka utaratibu Kwa wafungwa wa Tanzania Bara na Maabusu watakavyoruhusiwa kupiga kura siku ya Uchaguzi

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Cha wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba ameipongeza Tume Kwa utaratibu ambao wameuweka katika uchaguzi wa mkuu kwani itakuwa mara ya kwanza Kwa vyama vya Siasa kupewa orodha ya wapiga kura wa Nchi nzima kabla ya kuanza zoezi la Kampeni jambo ambalo hapo awali halikuwepo

Aidha Prof. Lipumba amesema kuwa wasiwasi wake upo Kwa mawakala ambao tume imewaeleza kuwa wataapishwa siku saba kabla ya uchaguzi jambo ambalo anaamini Tume haitaweza kuwaapisha mawakala wote kutokana na ufinyu wa muda