Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi, amesema miaka mitano ijayo ya Uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, itahakikisha inajenga Kongani ya Viwanda kwa ajili ya Usindikaji Vyakula na Maziwa, katika Jimbo la Kwela lililopo halmashauri ya Sumbawanga Vijijini.
Dkt Nchimbi ametoa kauli hiyo leo Septemba 08, 2025 akiwa katika Mji wa Laela, ikiwa ni muendelezo wa harakati za Kusaka kura kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuelekea Oktoba 29 mwaka huu.
Leave a Reply