Wasanii Waliochaguliwa kuwania tuzo za grammys 2026.

Tuzo za muziki za kimataifa za GRAMMYs 2026 zimezidi kuongeza hamasa barani Afrika, huku majina makubwa kutoka Afrika yakiingia kwenye kinyang’anyiro cha kipengele cha “Best African Music Performance.”

Hawa ndiyo wasanii walioteuliwa mwaka huu:

🎵 Love – Burna Boy 🇳🇬

🎵 With You – Davido 🇳🇬 & Omah Lay 🇳🇬

🎵 Push To Start – Tyla 🇿🇦 Ft Gunna 🇺🇸

🎵 Hope & Love – Eddy Kenzo 🇺🇬 & Mehran Matin

🎵 Gimme Dat – Ayra Starr 🇳🇬 Ft Wizkid 🇳🇬

Kipengele hiki kinaendelea kuonesha jinsi muziki wa Kiafrika unavyopata kutambuliwa kimataifa, huku wasanii wakitoka mataifa tofauti ya bara hili wakileta ladha ya kipekee katika muziki wa dunia.

Mashabiki wengi tayari wameanza kuonyesha hisia zao mtandaoni, wakipigia debe nyimbo na wasanii wanaowapenda, huku wengine wakisubiri kwa hamu kuona nani ataibuka mshindi katika usiku wa tuzo hizo maarufu duniani.