Watia nia viti maalum waliotoa Rushwa mara wawekwa mtu kati

TAKUKURU Mkoa wa Mara imekiri kuona kufuatilia na kuwakamata baadhi ya watia nia Udiwani Viti Maalum ambao baadhi yao wameonekana kwenye picha mjongeo (Video) wakigawa Fedha na Vitenge wakiwagawia Wajumbe.

Katika hatua hio TAKUKURU iliwakamata wanachama 7 nje ya ukumbi Wakiwa wanagawa fedha Musoma Vijijini, katika uchaguzi wa Udiwani viti maalum ambapo watano walikuwa wakitumia gari aina ya Noah kwa kusambaza fedha kwa wajumbe.

Akizungumza na Wasafi Media katibu wa CCM Mkoa wa Mara Ndg.Iddi Mkoa anaeleza kwa sasa Chama kipo kwenye mchakato wa vikao kwaajili ya kufanya mchujo na anaeleza ikigundulika kuna ukweli wowote kuhusiana na picha mjongeo hizo basi walengwa hawatateuliwa na chama kuwa viongozi.

Aidha jitihada za kuwatafuta walengwa walioonekana wakigawa Fedha na Vitenge kwa wajumbe ambao ni Bi. Herieth Makumira na Amina Masisa, Mmoja alikata simu baada ya kusikia ni mwandishi akizungumza na Bi. Amina alieleza kuwa habari hizo ni za uzushi.