Watu wasiojulikana wachoma moto Gari La mwenezi wa CCM mbeya mjini

Taharuki imetanda kwa familia ya katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbeya mjini baada ya watu wasiojulikana kuvamia nyumbaji kwake na kuchoma moto gari lake aina ya Nissan Xtrail.

Tukio hilo lililo tokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa kumi limeacha hofu kwa watu 11 waliokua ndani ya nyumba hiyo kutokana na moto uliokuwa ukiteketeza gari hilo kuanza kuchoma vitu vilivyokuwa kwenye nyumba waliyokuwa wamelala watu hao.

Akizungumza kuhusiana na tukio hilo nyumbani kwake katika mwenezi wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini Mng’ong’o amesema tukio hilo linakuja ikiwa ni wiki moja tuu imepita watu hao ambao bado hawajajulikana kuingia nyumbani kwake na kumuibia taili jipya la gari likiwa nyumbani kwake.