Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene,amezindua namba maalum itakayotumiwa na wananchi kufuatilia kitambulisho cha taifa baada ya kuwasilisha maombi ya kitambulisho hicho.
Akizungumza leo ,jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi huo amesema vitambulisho vingi vimezalishwa na tayari vimepelekwa sehemu husika ambapo muombaji alijiandikishia na bado wahusika awajafuata kadi zao.

“Hivi leo tunavyozungumza katika Wilaya zetu,viko vitambulisho vingi sana ambavyo havijachukuliwa na sababu kubwa inakua kwamba muombaji hajui kitambulisho chake kipo katika hatua gani,kupitia mfumo huu ambao ninauzindua utajibiwa na utaambiwa kama namba yako umepata ndani ya siku tano na kama ujapata ndani ya siku tano tangu ulipoomba ukitumia mfumo huu (15274) utajibiwa kwanini ujapata .” Amesema Waziri Simbachawene









Leave a Reply