Mbunge wa Jimbo la Mbogwe, Nicodemus Maganga, leo Juni 4, 2025, amesimama Bungeni jijini Dodoma kuchangia hoja ya Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2025/2026, akisisitiza umuhimu wa Serikali kuchunguza vyanzo vya mali zinazoshukiwa kuwa haramu.
Katika mchango wake, Mhe. Maganga alizungumzia suala la fedha haramu, akisema kuwa baadhi ya watu wanajenga maendeleo yao binafsi kwa kutumia fedha zinazotokana na udhurumu au biashara ya dawa za kulevya.
Mhe. Maganga, amesisitiza kuwa kuna kila sababu kwa Serikali kujua shughuli anazofanya mtu yeyote anayeonekana kufanya maendeleo makubwa.
Leave a Reply