Bilioni 67 zamvuta Philogene kujiunga na Ipswich

Jaden Philogene, winga mwenye umri wa miaka 22, anakaribia kujiunga na Ipswich Town kutoka Hull City kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kuwa pauni milioni 22 zaidi ya Tsh. bilioni 67. 

Philogene alijiunga na Hull City kutoka Aston Villa mnamo Septemba 2023 na alifunga mabao 12 katika mechi 32 za Championship msimu uliopita.

Kabla ya uhamisho huu, Philogene alikuwa akihusishwa na vilabu vingine kama Barcelona na Everton, lakini inaonekana ameamua kujiunga na Ipswich Town, ambao wamepanda daraja hadi Ligi Kuu ya England msimu huu. 

Kwa sasa, Philogene yuko katika hatua za mwisho za kukamilisha uhamisho wake, ikiwa ni pamoja na kufanyiwa vipimo vya afya na kukubaliana masharti binafsi na Ipswich Town.