Manchester City wamefikia makubaliano ya awali na beki wa kati wa Palmeiras, Vitor Reis, mwenye umri wa miaka 18, pamoja na wakala wake kuhusu masharti binafsi ya mkataba. Kwa sasa, mazungumzo yanaendelea kati ya Manchester City na Palmeiras ili kukamilisha uhamisho huo.
Manchester City wanajiandaa kutoa ofa ya takribani euro milioni 40 zaidi ya Tsh bilioni 122 kwa ajili ya kumnunua Reis.
Vitor Reis, aliyezaliwa Januari 2006, huko Santana, Brazil, alianza safari yake ya soka katika Academy ya R10 kabla ya kujiunga na Academy ya Palmeiras mwaka 2016 akiwa na umri wa miaka 10.
Katika msimu wa 2024, Vitor alipandishwa hadi timu ya wakubwa ya Palmeiras, akicheza mechi 8 na kufunga bao 1 katika ligi ya Serie A ya Brazil.
Pia amewakilisha timu ya taifa ya Brazil katika ngazi za vijana, ikiwa ni pamoja na kikosi cha chini ya miaka 17.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.