Rodriguez ajiunga na Club Leon ya Mexico

Nahodha wa timu ya Taifa ya Colombia, James Rodriguez (33) amejiunga na Klabu ya Liga MX ya Mexico, Club Leon akitokea Rayo Vallecano ya LaLiga kwa uhamisho wa bure.

Ripoti za vyombo vya habari vya ndani zilisema Rodriguez amesaini mkataba wa mwaka mmoja na chaguo la kuongeza mwaka mwingine.

“Rayo Vallecano de Madrid na Club Leon ya Mexico wamefikia makubaliano ya uhamisho wa James Rodriguez, tunamtakia James mafanikio mema katika hatua yake mpya,” taarifa ya klabu ya Rayo.