Watu 15 wakamatwa kwa Wizi wa Mali kwenye Ajali Mbeya

Watu 15 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kupatikana na Shehena ya unga wa sembe ambayo ina kilo zaidi ya 1000 baada ya gari lilikouwa likisafirisha unga wa sembe kupata ajali katika Wilaya ya Rungwe.

Baada ya ajali hiyo, wananchi wa Kijiji cha Kanyegele na Vijiji jirani vya Mpandapanda na Igula walifika eneo la ajali na kuanza kuiba Unga wa Sembe uliokuwa kwenye mifuko ya kilogramu 25 ipatayo 1253 na kutoweka nayo wakitumia usafiri wa Pikipiki maarufu bodaboda.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Mussa Zacharia Mwile na wenzake 14 wakiwa na vielelezo Unga wa Sembe ulioibwa mifuko 65 mizima na minne ikiwa nusu, turubai mbili za gari hiyo pamoja na Pikipiki saba zilizokuwa zikitumika kubeba na kusafirisha mali hiyo ya wizi.