Familia ya John Mushi mkazi wa Sambarai Kibosho wilayani Moshi mkoani kilimanjaro imepata furaha baada ya mke wake Maria Mushi kujifungua watoto wa nne usiku wa kuamkia Januari 10 katika hospitali ya rufaa KCMC Mjini Moshi

Watoto hao wawili wa kiume na wawili wa kike bado hawajapewa majina wapo hospitalini chini ya uangalizi wa madaktari.

Licha ya furaha ya kuwapata watoto hao, familia hiyo imeomba msaada wa malezi kwa serikali, taasisi na watu binafsi kwani wanasema tayari wana watoto wanne wengine na hivyo sasa wana watoto nane na hawana kipato cha kutosha.

Leave a Reply