Watatu wakamatwa wakiiba Nondo za Shule Gairo

Kamati ya Usalama Wilaya ya Gairo ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo ndugu Jabiri Makame imewakamata watu watatu akiwemo John Mbaluka, Petro Mauji na Mnyandwa Letema kwa tuhuma za Wizi wa Nondo 10 ambazo ni Mali ya Serikali kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Amali inayojengwa Kijiji Cha Kwipipa Kata ya Iyogwe.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo ndugu Jabiri Makame wakati wa Ziara ya Kamati ya Usalama wakati wa Kukagua Maendeleo ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Gairo. Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ameagiza Jeshi la Polisi kuwahoji Watunza Stoo, Mafundi na watu wengine wote watakaosaidia kukamilika kwa upelelezi wa tuhuma hizo na Kisha kufikisha suala hilo Mahakamani.

Wilaya ya Gairo inatekeleza Miradi ya Maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 6 zilizopokelewa katika nusu ya kwanza ya Mwaka wa fedha 2024/2025.