Mashangazi waonywa kutumia Mikopo ya 10% Kuwalea Vijana

Mkuu wa wilaya ya Sikonge Bw. Cornel Magembe amepiga marufuku tabia za vijana na kina mama maarufu kama mashangazi kutumia pesa za mikopo ya halmashauri kama vishawishi vya kuwapata wapenzi wapya.

Magembe ametoa kauli hiyo kwenye hafla ya kukabidhi fedha za mikopo kwa vikundi 55 vilivyokidhi vigezo ambapo jumla ya shilling million 460.49 zimetolewa na halmashauri ya wilaya ya Sikonge ikiwa ni kiasi kilichotengwa kutoka aslimia 10 ya mapato yake.

Hayo yanafuatiwa na utamaduni uliyobainika ambapo vijana wanatajwa kushindwa kurejesha mikopo kutokana na kutumia fedha hizo kuongeza wanawake na kinamama hutumia fedha hizo kama ndoano ya kuwanasa vijana wadogo katika ugo wa mahusiano.