Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Victoria ambaye pia ni mtia nia wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa Ezekia Wenje amewataka wanachama wa Chama hicho kufanya kampeni za kistaarabu, huku akisisitiza kuwa katika kampeni zake hataruhusu mtu yoyote ambaye anamuunga mkono kwenye Uchaguzi huo, kuanza kutukana viongozi wengine.
Wenje amebainisha hilo Leo Januari 16, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea ndani ya Chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Chama hicho.
“Sisi katika kampeni yetu hata Mwanza nilisema, sitaruhusu mtu yoyote anayeniunga mkono kwenda kumtukana mtu mwingine kwasababu uchaguzi unaisha Tarehe 21 tu na maisha yatasonga, Leo ukimtukana mtu sana alafu kesho anakuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa au Makamu Mwenyekiti wa chama unafanyake naye kazi?, nawaomba tufanye kampeni za kistaarabu kwasababu mwisho wa siku tunajenga chama kimoja,” amesema Wenje.
Leave a Reply