Mshambuliaji wa Real Madrid, Endrick (18) kutoka Brazil ambaye aliipa ushindi Madrid kwenye mchezo wa jana wa Cop Del Rey kwa kupachika magoli mawili kambani kati yangu matano yaliyofungwa na Timu yake amesema kuwa anaamini Kocha wake Carlo Ancelotti hafanyi maamuzi ambayo ni bora kwake bali maamuzi bora kwaajili ya Madrid.
Endrick katika mchezo wa jana dhidi ya Celt Vigo aliingia uwanjani dakika ya 79 ya mchezo wakati matokeo ya mchezo huo yakiwa ni 2-2 ndipo alipofanikiwa kufunga magoli mawili baada dakika 30 za nyongeza baada ya zile 90 kukamilika kwa sare.
“Sikutarajia kucheza dakika zaidi dakika nilizopata, Ancelotti anajua anachofanya, Hafanyi kile ambacho ni bora kwangu, lakini kwaajili ya timu. Ikiwa timu itamuhitaji Kylian, Vini, au Rodrygo, watakuwepo, Ikiwa ni Arda Güler, atakuwepo. Ikiwa ni mimi, nitakuwepo.” alisema Endrick.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.