Majaji na Mahakimu wanawake  washiriki riadha kupinga ukatili wa kijinsia.



Zaidi ya washiriki 200  kutoka  Chama cha majaji na mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA), wameshiriki mbio maalumu kwa ajili ya kutoa elimu ya  kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia hasa katika kuelelekea maadhimisho ya miaka 25 ya Chama hicho.



Mbio hizo zimefanyika jijini Arusha zikiongozwa na Mwakilishi wa spika wa bunge la Tanzania Shally Raymond ambaye ni mwenyekiti wa wabunge wanawake.

Anasema ni muhimu kuwa na tafakari ya pamoja changamoto zinazowakabili jamii katika masuala ya ukatili hasa kwa wanawake na watoto ambao wanaomekana Bado wapo nyuma katika kulinda na kutetea masuala ya kijinsia .




Mbio hizi zimehusissha Kilomita 5, 10 na 21 ambapo Jaji Barke Sehel ni Mwenyekiti wa TAWJA anasema mbio hizi zimelenga kuongeza uelewa kwa Jamii kuhusu Haki za Kijinsia, na hatua za kuchukua dhidi ya unyanyasaji kwa makundi ya  Wanawake na Watoto.

Profesa Ibrahimu Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania ni miongoni mwa Viongozi Wakubwa wa Nchi walioshiriki Mbio hizi.