Meneja wa Aston Villa, Unai Emery anasema timu imejipanga kuhakikisha inafuzu moja kwa moja kwenda hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.
Aston Villa wako kibaruani leo Januari 21, 2025 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Monaco ikiwa ni mechi muhimu kwa wote wawili kujihakikishia wanajikita katika nafasi nane za juu kwenye msimamo huo.
Ikumbukwe kuwa Aston Villa wamerudi tena kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 42 na wako katika nafasi nzuri ya kumaliza katika nafasi ya nane bora, wakiwa katika nafasi ya tano kwa alama 13 huku zikiwa zimesalia mechi mbili.
“Nadhani tuna ari kubwa kucheza Ligi ya Mabingwa kwa sababu klabu haikucheza kwa muda mrefu, tunataka kushindana tukijaribu kuwa bora kwenye mchezo huu, tuna nafasi kubwa sana ya kufanikiwa.
“Nadhani tunahitaji alama tatu au nne zaidi ili kupata nafasi ya nane bora, lengo letu ni kuwa ndani ya nane bora na kesho,” alisema Emery.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.