Kanye West Amtaja North Kama Sababu Ya Kuupenda Muziki Tena

North West, binti wa miaka 11 wa Kanye West, anaonekana kuonyesha hamu kubwa ya kufanya muziki kama baba yake. Kanye alieleza kwenye Instagram jinsi North alivyomfanya kuamsha upendo wake wa kutengeneza muziki kwa kumtaka amtengenezee beats kwa ajili ya albamu ya #BULLY.

“Mtoto huyu mdogo amenifanya nipende muziki tena Aliniomba nimtengenezee beats, nikaamua kutumia ASR na kukata beats kwa mikono yangu kwa ajili ya albamu ya BULLY.” Aliandika Kanye

Kutoka kwenye familia yenye historia ya ubunifu, North anaweza kuwa kipaji kingine kitakachochangia kwenye ulimwengu wa muziki. Mashabiki wanasubiri kuona ikiwa ataendeleza urithi wa baba yake.