Chris Brown Aishtaki Kampuni Ya Warner Bros. Discovery Kwa Kumchafua, Adai Trilioni 1.2/= .

Chris Brown Hacheki Yeyote! Kwani Amewashtaki Watayarishaji Waliopanga Kuachia Documentary Ya Unyanyasaji Wake Iliyopewa Jina La “Chris Brown: A History Of Violence”, Akidai Kuwa Documentary Hiyo Inasambaza Madai Ya Uongo Kumhusu Yeye.

Kwa Mujibu Wa nyaraka za mahakama Zilizonaswa na TMZ, Brown anaituhumu Warner Bros. Discovery na wengine kwa Kumchafua, licha ya kutoa “ushahidi” Lakini madai hayo ni ya uongo. Breezy Anasema Kwamba Hajawahi kupatikana na hatia ya Unyanyasaji wowote ule wa kingono Huku akilaani Series Hiyo Inayomuonesha kama “mbakaji wa mara kwa mara na mnyanyasaji wa kingono.”

Pia Amesema Moja Ya Kesi Yake Kubwa Iliyowekwa Katikati Ya Series Hiyo Ilitupiliwa Mbali mahakamani kutokana na madai ya uongo. Hivyo Anadai Fidia Ya Kiasi Cha $500m (Tsh Trilioni 1.2/=) Kwa Kumchafua.

Kisa maarufu cha unyanyasaji kilichomhusisha Chris Brown kilitokea mwaka 2009 alipomshambulia aliyekuwa mpenzi wake, Rihanna, tukio lililosababisha Rihanna kulazwa hospitalini kwa majeraha ya usoni.

Tangu tukio hilo, Chris Brown amekuwa akikumbwa na migogoro ya kisheria na wasanii wenzake, mashitaka ya unyanyasaji, pamoja na amri ya mahakama ya kutoonana na aliyekuwa mpenzi wake baada ya kunaswa vitisho vya ujumbe wa simu na sauti.