Rais Samia aipandisha Hadhi Kibaha Mjini Kuwa Manisapaa

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ameridhia Halmashauri ya Mji Kibaha iliyopo Mkoani Pwani kupandishwa hadi na kuwa Manispaa.

Uamuzi huo umetangazwa leo Januari 27 na Waziri wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa Mjini Kibaha.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa akizungumza katika mkutano wa CCM uliofanyika Januari 27 katika viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.

Mchengerwa, ametangaza hilo wakati akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na Wananchi katika mkutano mkubwa wa kuunga mkono maazimio ya mkutano Mkuu wa CCM Taifa uliomteua Rais Samia kuwa mgombea wa Urais mwaka 2025