Staa wa muziki na mjasiriamali Rihanna amejitokeza kukanusha video iliyosambaa kwenye Instagram ikimwonyesha akizungumza kuhusu manunuzi yake ya vitu vya gharama kubwa. Video hiyo, ambayo ilitumia akili bandia (AI) kuiga sauti yake, haikuwekwa wazi kuwa ni ya AI, jambo lililowafanya mashabiki wengi kuhoji uhalisia wake.
Rihanna mwenyewe alitoa maoni yake kwenye video hiyo, akiandika, “Who tf is this talking??!” akionyesha kushangazwa. Mashabiki wake pia walionyesha mashaka yao, wakisema #Rihanna wa kweli hawezi kujisifu kwa mali zake.
Hii si mara ya kwanza sauti ya Rihanna kutumiwa na AI bila ruhusa yake. Mwaka 2023, wimbo bandia wa Rihanna na #BadBunny ulisambaa kwenye #SoundCloud, kama ilivyotokea kwa wimbo wa AI wa #Drake na #TheWeeknd.
Hata hivyo, mashabiki wa Rihanna wataweza kumsikia kwa sauti yake halisi kwenye filamu mpya ya #Smurfs, ambapo atacheza kama Smurfette. Trela ya filamu hiyo, inayotarajiwa kutoka Julai mwaka huu imeshatolewa.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.