Kiungo wa Manchester United, Casemiro amesema msimu wake bora kuwahi kutokea kwenye maisha yake ya soka ni ule msimu ambao alijiinga na Manchester United.
Casemiro amesema licha ya kucheza Real Madrid na kutwaa makombe ya #UCL anadhani kucheza Old Trafford ni bora zaidi kwenye maisha yake ya soka.
“Mmoja wa msimu wangu bora kama mwanasoka ulikuwa wa kwanza na Man United, sisemi kwa maana ya kuwa na mataji kama UCL nikiwa na Madrid, lakini kama mchezaji, nadhani Old Trafford imenipa toleo bora zaidi la Casemiro katika mwaka wangu wa kwanza,” alisema Casemiro.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.