Kocha wa Namungo “Juma Mgunda” alikuja na majibu sahihi ya maswali ya Simba SC

Jean Charles Ahoua akifunga penati

Anaandika Kelvin rabson

Nafikiri kocha wa Namungo “Juma Mgunda” alikuja na majibu sahihi ya maswali ya Simba , hakuhitaji kupishana kiwanjani muda mwingi aliwapa Simba umiliki wa mpira huku wakiweka mtego kwa kuunda mashambulizi kwa kushtukiza (Counter Attacks) …. Kipindi cha kwanza walifanikiwa wapi ?

Namungo walizuia wakiwa chini kwenye “Low block” tena wakiwa karibu karibu hakuna nafasi kati ya walinzi na viungo wao na kufunga njia za kupitisha mpira , kuna nyakati viungo wa Simba wakipokea mpira kwenye zone ya 14 hawaelewi nini wakifanye : hawakufanya machaguo sahihi ya pasi zao , maamuzi yao mengi hayakuwa sahihi then hakuna runners eneo la mwisho …. How?

Kwasababu Namungo walitoa majibu sahihi kwenye maswali ya Simba hasa pale wasipokuwa na mpira ….. kuwafanya Zimbwe na Kapombe wasipate nafasi kubwa nyuma ya defense yao huku hakuna nafasi kwa mawinga wao kushambulia zile “Half Spaces” baada ya hapo Simba walichagua njia gani ?

1: Kushambulia kwa kutumia mipira mirefu (Long Balls) kupiga nyuma ya walinzi wa Namungo .

2: Kutumia mipira iliyokufa (Set pieces) na walifanikiwa : Tukio la kwanza la Penalti .

Kipindi cha Pili

Simba walibadilisha aina ya uchezaji wao kwa muundo wa 2-2-4-1 , kilichobadilika ni Simba kufanya mpira utembee kwa haraka zaidi , runners eneo la mbele + idadi nzuri ya wachezaji eneo la pambeni (Kapombe na Zimbwe wanakuwa pembeni kabisa ya uwanja then mawings wao mda mwingi wanakuwa ndani kwenye “Half spaces” kuwafanya FBs wao kufanya runners za hatari nyuma ya defense ya Namungo : nafasi zikaanza kufunguka kwa Simba .

Note

1: Kapombe “Good Gam, Position yake , Movements (Runs za kushambulia nyuma ya Mlingo)

2: Jean Ahoua Magoli 10 mpaka sasa kwenye NBCPL .

3: Ile Red Card ya Mkombozi ( refa anajua yeye)

4: Combo ya Kagoma na Ngoma inawapa Simba msingi muhimu wa kuunda mashambulizi kuanzia chini

5: Najim akiwa na mali ana imani sana na kipaji chake

FT : Namungo 0-3 Simba .