Kumbusu Mtu bila hiyari yake ni Ukatili wa kijinsia – Waziri Mkuu



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametumia jukwaa la uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoani Lindi, kukumbusha kuhusu ukatili wa aina mbalimbali kwenye jamii, akikumbusha kuwa Ukatili wa Kijinsia na kingono ni pamoja na kumbusu mtu akiwa hayupo tayari na kutumia maneno ya kumshawishi mtu ilihali ikiwa hayupo tayari.

Aidha Pia Waziri mkuu Mhe. Majaliwa amezungumzia kuhusu Ukatili wa teknolojia, akisema kuvujisha picha za mtu za faragha, kuvujisha mitandaoni taarifa binafsi za watu pamoja na kusambaza picha za kubuni zenye kufanana na uhalisia ni miongoni mwa mambo mengine yenye kuhesabika kama makosa ya ukatili wa kijinsia.

Waziri Mkuu pia ambaye amekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hiyo, amekemea tabia za kushusha heshima na thamani ya mtu, kuita watu majina mabaya, kumuaibisha mtu, lugha za matusi, fedheha pamoja na tamaduni za utakaso zinazofanywa na baadhi ya jamii kwa akinamama wajane ambao hutafutiwa waume na baadhi ya ndugu wa marehemu pale mume wake anapotangulia mbele za haki.

@Barakadon_
#WasafiDigital