Burna Boy Aongelea Umuhimu Wa Tuzo Za Grammy

Muimbaji Wa Nigeria #BurnaBoy Kwenye Mahojiano Na Jarida La “Billboard France” Wiki Iliyopita Amezungumzia Zaidi Kazi Yake Ya Muziki Ikiwemo Umuhimu Wa Tuzo Kubwa Za Muziki Duniani Za #Grammys .

Burna Boy anasema kwamba ushindi wake wa Grammy unawakilisha kujiamini, kuvuka mipaka, na kuthibitisha ukuaji wa muziki wa Afrika kimataifa.

Burna Boy, ambaye ni mmoja wa wasanii wakubwa wa Afrobeats, amesema ushindi wake haukuwa tu kwa ajili yake binafsi bali kwa bara zima la Afrika. Ameeleza kuwa mafanikio haya yanaonesha jinsi muziki wa Kiafrika unavyoendelea kukua na kupata ushawishi mkubwa duniani kote.