•Hungary kufungua ubalozi mdogo Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Hungary zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya Ushirikiano katika eneo la Mafunzo ya Kidiplomasia.
MoU hiyo inalenga kubadilishana ujuzi na uzoefu pamoja na kubadilishana wanafunzi wa diplomasia ili kupata elimu itakayokidhi uhitaji wa sasa ambapo wadau wakuu ni Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim kwa upande wa Tanzania na Chuo cha Diplomasia cha Hungary.

Hati hiyo imesainiwa jijini Budapest, Hungary na Waziri wake Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary, Mhe. Péter Szijjártó.

Aidha, kufuatia kuimarika kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Hungary na mwaliko kutoka Serikali ya Tanzania, Hungary imeridhia kufungua Ubalozi Mdogo jijini Dar es Salaam mwezi Septemba utakaosaidia kuimarisha zaidi ushirikiano na Tanzania. Akizungumza hayo, Mhe. Waziri Szijjártó amebainisha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za kipaumbele barani Afrika kwa Hungary.
Leave a Reply