Rais Samia azidi kuboresha sekta ya Afya, Elimu mkoani Tanga

Zahanati iliyopo katika Shule ya Wasichana Tanga imeleta mchango mkubwa katika utoaji wa huduma za afya kwa wasichana na jamii kwa ujumla ambao hatua hiyo ni matokeo ya juhudi za pamoja kati ya serikali katika kuboresha sekta ya elimu na afya.

Rais Samia ameonyesha msaada wake kwa sekta ya afya kwa kuweka vifaa vya kisasa vinavyosaidia katika utoaji wa huduma bora. 

Uwekaji wa mashine hizo muhimu unalenga kuongeza ufanisi na usahihi katika utambuzi na matibabu ya magonjwa mbalimbali ikiwa ni mkakati wa serikali wa kuboresha miundombinu ya afya katika shule na vituo vya afya vijijini na mijini.

Katwila Shule ya Wasichana Tanga, Mashine Muhimu Zilizowekwa ni pamoja na TPC (Therapeutic Positive Pressure Cycle), Patient Monitor, Sanction Machine, ECG na Electro Cardio Machine.

Kituo hicho kinaweza sasa kufanya vipimo vya malaria, HIV na ujauzito. Uwepo wa maabara ya kisasa unafanya iwezekane kuchunguza na kugundua magonjwa mapema.