Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ubongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI) imepanga kuanzisha benki ya mifupa ili kuboresha huduma za tiba ya mifupa kwa gharama nafuu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema benki hiyo itahakikisha wagonjwa wanapata mifupa kwa upandikizaji kwa njia salama na yenye ufanisi.
Mifupa itakayohifadhiwa kwenye benki hiyo itakusanywa kwa utaratibu maalum na itapimwa ili kuhakikisha haina magonjwa kabla ya kuhifadhiwa,.
Hata hivyo, alibainisha kuwa huduma hiyo haiwezi kuanza bila kupitishwa kwa Sheria ya Upandikizaji wa Viungo na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Alisema sheria hiyo ni muhimu ili kuweka utaratibu rasmi wa ukusanyaji na utunzaji wa mifupa kwa matumizi ya kitabibu.
Leave a Reply