Offset Amuita Elon Musk Mbaguzi Wa Rangi.

Rapa Wa Marekani Offset Amuita bilionea Elon Musk “Mbaguzi” (Racist B*tch) baada ya ripoti kuibuka kuwa Musk anataka Trump Amsamehe Derek Chauvin, afisa wa zamani wa polisi aliyehukumiwa kwa mauaji ya George Floyd. Hivyo Offset Ameonesha Kutokubaliana Na Mawazo Ya Bilionea Huyo.

Maoni Ya Elon Musk Akitaka Derek Chauvin Apewe Msamaha
Maoni Ya Offset Baada Elon Musk Kuonekana Akiunga Mkono Derek Chauvin Aachiwe Huru

Kumbuka Derek Chauvin alihukumiwa kwa kosa la mauaji ya George Floyd (Mmarekani Mweusi) mwaka 2020, tukio lililochochea maandamano makubwa ya Black Lives Matter (BLM) duniani kote. Musk, ambaye ni mmiliki wa X (zamani Twitter), ameripotiwa kuunga mkono msamaha kwa Chauvin, jambo ambalo limezua Mijadala mtandaoni.

Hadi sasa, Elon Musk Bado hajajibu Chochote Kwa Offset, Lakini Mada Hii Inaendelea Ku-trend Mitandaoni Huku Watu Mbalimbali Wakitoa Maoni Yao Juu Ya Suala Hili.