Wanawake wajasiriamali Arusha wamkaribisha Rais Samia kwa kishindo

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wanawake wa Mkoa wa Arusha wameonesha shauku ya kumwona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na umahiri wake wa uongozi aliouonesha.

Wamesema kutokana na ujasiri wake, umewapa nguvu ya kuanzisha Miradi mbalimbali ya kiuchumi ambayo inawasaidia kuendesha maisha yao.

Rais Dkt Samia Suluhu anatarajia kuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani ambayo itaadhimishwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Machi 8, 2025.