Tory Lanez Atumia “AI” Sauti Ya Trump Kwenye Album Yake Mpya.

Tory Lanez Bado Hajakata Tamaa Na Kesi Yake! Kwani Ametumia Sauti Ya “AI” Ya Rais Wa Marekani Trump Katika Album Yake Mpya, Akidai Kuwa Yeye Ndio Aliyezuia Megan Kupigwa Risasi Na kuhakikisha kwamba Kelsey Nicole haendi jela.

Sauti Hiyo Ya Trump Iliyopo Kwenye Outro Ya Album Yake Mpya “Peterson” Imesikika Ikisema 👇

“Unafahamu tatizo kwenye hili sakata zima la Tory Lanez ?
Ni kwamba wamemfanya kuwa muhanga kwa kutomlinda Mwanamke Mweusi, Lakini Jambo ambalo wanasahau ni kamba Tory Lanez aliwalinda wanawake weusi wawili Usiku ule, Mmoja asiende jela na mwingine asipigwe Risasi. Nadhani ni Muda wa Kumtoa Jela” – Sauti Ya (AI) Ya Trump Kuhusu Kutoa Tory Jela Ambaye Anatumikia Kifungo Cha Miaka 10.

Mashairi Ambayo Tory Ametumia AI Kuweka Sauti Ya Trump Kwenye Album Yake Mpya Mwisho Mwa Ngoma Yake Iitwayo “My Shayla”

Hata Hivyo Kauli Ya Tory Kudai Alimsaidia Megan Na Kelsey Imeleta Utata, kwani Lanez alikutwa na hatia ya kumpiga risasi Megan 2020, Licha Ya Kusisitiza kuwa hana hatia, Lakini madai haya mapya yanaibua maswali zaidi kuhusu kile kilichotokea usiku huo.

Je, Tory Lanez alikuwa mpatanishi au mtuhumiwa mkuu wa tukio hilo? Wengi Wapo Njia Panda, huku wengine Wakiungana Nae, Wengine Wakiona Anakandamizwa Na wengine wakiona ni mbinu ya kusafisha jina lake kupitia muziki wake. Ila Muda Ndio Utasema !.