Burna Boy Alirekodi Hitsong Yake “YE” Akiwa Bar Amelewa.

Burna Boy Alivyoeleza namna ambavyo ngoma yake #YE ilitengenezwa. Kwenye mahojiano Aliyowahi Kufanya Na “Rap Radar” mkali huyo wa Afrika Alisema Kwamba alirekodi mkwaju huo akiwa bar na amelewa kinoma.

Amesema alienda kwenye Bar ya Mshikaji Wake aitwaye Shina Peller ambapo akiwa amelewa tayari na hataki kusikia chochote kinachohusu muziki, Shina Peller alikuja na simu na kisha kumsikilizisha mdundo mkali sana. Baadaye walipanda juu ambapo kuna studio ya kiaina na haikumchukua hata dakika 10 kuikamilisha “YE”.

Ndio maana ndani utasikia kamtaja Shina Peller “Shout out Shina Peller, That’s my bro, my family.”🔥🎶.

Ye Ni Ngoma Ambayo Imemtambulisha #BurnaBoy Kimataifa Zaidi, Wasanii Kama Kanye West, Rihanna, Neymar Walikutwa Mara Kadhaa Wakiisikiliza Na Kuruka Nayo.