Jeshi la Polisi mkoa wa Geita linawashikilia watu kumi na mmoja kwa tuhuma za kukutwa na laini 9389 za mitandao mbalimbali ya simu walizokuwa wakitumia kufanyia halifu kwa njia ya mtandao na unyang’anyi.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi wa Mkoa wa Geita kamishina Msaidiizi wa polisi ( SACP) Safia Jongo amesema Watuhumiwa hao walikamatwa Machi 13, 2025, katika Kata ya Ludete, Wilaya ya Geita, baada ya polisi kupata taarifa na kuweka mtego uliofanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao
Watuhumiwa hao wamekutwa na vifaa mbalimbali vya kufanyia uhalifu
ikiwemo Laptop moja aina ya HP, Mashine mbili za kusajili line kwa kutumia alama za vidole, Simu janja “Smartphone” 15, Simu ndogo za kawaida 18, Sim card mpya za mitandao mbalimbali 1600, Mabaki ya Sim card za mitandao mbalimbali jumla 6189, Line za Yass (Tigo) zilizosajiliwa 2600 na Begi tatu za mgongoni.
Watuhumiwa hao ni llege Charles (42), Shabani Abdallah (25), Daudi Omary
(25), Alex Rashid (32), Jumanne Mageso (27), Meshack Bahebe (31), Alex Edward (29), Nkwabi Ipilinga (21), Dennis Ndihunze (33), Vicent Vedastus
(25) na Hamduni Issa (30).
Jeshi la Polisi linaendelea na chunguzi kwa kushirikiana na taasisi nyingine ili kuweza kubaini mtandao mima wa wahalifu hao na kuwachukulia hatua
kali za kisheria.
Leave a Reply