Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Mwenendo wa viashiria vya uchumi na bajeti katika mwaka 2024/2025 umeendelea kuwa wa kuridhisha ambapo Katika mwaka 2024, Pato halisi la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 5.5 ikilinganishwa na asilimia 5.1 mwaka 2023.
Majaliwa ameeleza hayo wakati anawasilisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2025/2026 leo Bungeni jijini Dodoma ambapo amesema Ukuaji huo ulitokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme; uimarishaji wa huduma za jamii; kuongezeka kwa mikopo kwa sekta binafsi iliyochachua shughuli za kiuchumi; kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji; na kuimarika kwa sekta ya uchukuzi.
Aidha, sekta zilizokuwa na kiwango kikubwa cha ukuaji katika kipindi cha marejeo ni pamoja na shughuli za sanaa na burudani asilimia 17.1, fedha na bima asilimia 16.3, na habari na mawasiliano asilimia 14.3″
Unaweza Kutazama Hotuba Yote kupitia YouTube | Wasafi Media
2024 Pato la Taifa lilikua kwa Asilimia 5.5 – Waziri Mkuu Majaliwa

Leave a Reply