Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameagana na Rais wa Jamhuri ya Angola, Mheshimiwa João Manuel Gonçalves Lourenço, wakati akihitimisha ziara yake ya kiserikali mjini Luanda, nchini Angola, tarehe 9 Aprili 2025.
Rais Samia alianza ziara hiyo tarehe 7 Aprili 2025, na ameikamilisha leo baada ya kutembelea kiwanda cha kusafisha mafuta cha Zanangol, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Tanzania kujifunza kutoka kwa Angola kuhusu maendeleo katika sekta ya mafuta — sekta ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi hiyo.
Aidha, katika kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Angola, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza rasmi kuondolewa kwa sharti la kulipia visa kwa raia wa Angola wanaotaka kuingia Tanzania, kama ishara ya kuendeleza mahusiano ya kirafiki na kiuchumi. Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa Serikali ya Angola kuondoa masharti hayo kwa Watanzania tangu mwaka 2024.
Rais Samia ahitimisha Ziara ya Kiserikali Nchini Angola

Leave a Reply