Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga na dereva wake wamefariki dunia kwenye ajali ya gari wakiwa njiani kutoka mkoani Mwanza wakielekea wilayani Bunda Mkoa wa Mara.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo usiku wa kuamkia leo Aprili 13, 2025 ambapo amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari hilo la Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kushindwa kumudu gari alipokuwa akimkwepa mwendesha baiskeli na hivyo kugongana na lori uso kwa uso.
Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda.
Poleni kwa msiba mungu alaze pema peponi roho za marehemu