Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza rasmi utekelezaji wa marufuku ya uingizwaji wa Mazao ya kilimo kutoka nchi za Malawi na Afrika Kusini, ikiwa ni hatua ya kulinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara wa Kitanzania kufuatia uamuzi wa nchi hizo kuzuia mazao ya kilimo kutoka Tanzania kuingia katika nchi zao.
Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ametangaza kuwa kuanzia leo Aprili 23, 2025 ni marufuku mazao yote ya kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini kuingia nchini, Pia ni marufuku Mazao ya kilimo kutoka katika nchi hizo kupita ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Pia, Bashe amesema Mahindi yote ambayo Malawi iliyanunua Tanzania kwaajili ya kutatua tatizo lao la njaa hayatapelekwa
Vilevile Tanzania haitaruhusu mbolea yoyote kutoka hapa nchini kwenda Malawi.
Leave a Reply