Diamond Mfalme Wa Youtube Africa.

Msanii Wa Muziki Africa SIMBA 🦁 @diamondplatnumz Ameweka Historia Ya Kuwa Msanii Wa Kwanza Na Wa Pekee Kutoka Afrika Ukanda Wa Jangwa La Sahara Kufikisha Subscribers Milioni 10 YOUTUBE.

Hivyo Diamond Anatarajia Kupokea Tuzo Ya ‘Diamond Play Button” Inayotolewa kwa chaneli Zilizofikisha au kupita subscribers milioni 10 Youtube, Ambayo Pia ni alama ya mafanikio makubwa kwenye Upande Wa Digital. Tuzo hii itakuwa ni utambuzi wa juhudi na ubunifu Wake ambao umemsaidia kuwa msanii anayeng’aa kimataifa.

Mafanikio haya yanamuweka Diamond kwenye nafasi ya kipekee sio tu ndani ya Tanzania au Afrika Mashariki, bali pia kimataifa, ambapo wasanii watatu tu wa Kiafrika wameweza kufikia kiwango hiki kwenye YouTube, ambao ni Mohamed Ramadan (Egypt 🇪🇬), Saad Lamjarred (Morocco 🇲🇦) na Soolking (Algeria 🇩🇿).

Hii Itakuwa Ni Alama Ya Uthibitisho Kwa Mashabiki Ambao Wamekuwa Wakim-Support Ndani Ya Miaka 15 Kwenye Muziki Wake na kumfanya kuwa moja ya wasanii vinara wa YouTube Africa. Lakini Pia Kwa kipindi Kirefu Diamond amekuwa akiongoza kuwa na watazamaji wengi youtube kwa afrika mashariki na kati Kiujumla.