Bunge la Ulaya limeitaka Tanzania kuhakikisha haki inatendeka katika kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, na kumuachia huru. Wabunge wamesisitiza umuhimu wa kesi hiyo kuendeshwa kwa uwazi, huku wakihimiza mamlaka za Tanzania kulinda uhuru wa kisiasa, usalama wa waandishi wa habari, na watetezi wa haki za binadamu kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.
Aidha, Bunge hilo limetoa wito kwa Tanzania kuweka mazingira rafiki kwa Vyama vya upinzani ikiwemo CHADEMA kushiriki uchaguzi wa mwaka huu 2025
Tundu Lissu anakabiliwa na mashtaka mawili, la uchochezi na la uhaini ambalo adhabu yake ni kunyongwa endapo atakutwa na hatia.
Leave a Reply