Tanzania na Finland kuendeleza Ushirikiano

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema wamefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Finland, Alexander Stubb, yanayolenga kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Finland uliotengenezwa miaka 60 iliyopita.

Rais Samia ameyasema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu Jijini Dar es Salaam, baada ya kumpokea mgeni wake huyo aliyewasili kwa ajili ya ziara ya siku tatu, ambapo pia ameongeza kuwa Nchi zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano kwa kuongeza mahusiano ya kiuchumi na kuchunguza njia mpya za ushirikiano katika maeneo ya Misutu, Madini, Uchumi wa Buluu, Elimu, na maeneo yenye maslahi ya pamoja.

Kwa upande wake Rais wa Finland Alexander Stubb amesema amefurahi kuja tanzania kwa mara nyingine kwani alikuja mwaka 2013 akiwa waziri wa biashara, hivyo ameahidi kuendeleza ushirikiano wa Tanzania katika sekta mbalimbali.