Waziri wa Mawsilano ya Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry Slaa leo Mei 16, 2025 amewasilisha bungeni bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo ameliomba Bunge kuidhinishiwa jumla ya feda Shilingi 291,533,139,000 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara hiyo.
Matumizi ya kawaida katika mwaka wa fedha 2025/26 Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inakadiria kutumia Shilingi 14,485,656,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, na kati ya fedha hizo Shilingi 6,958,609,000 ni kwa ajili ya Mishahara (PE) na Shilingi 7,527,047,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC).
Pia Mhe. Slaa, amesema matumizi ya miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2025/26 Wizara inakadiria kutumia Shilingi 277,047,483,000 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo Shilingi 98,480,905,000 ni fedha za ndani na Shilingi 178,566,578,000 ni fedha za nje.
Leave a Reply