Nyuki wamezua Kizaazaa kwa Wananchi katika Manispaa ya Singida kiasi cha kusimamisha Shughuli kwa Muda wa Zaidi ya saa nne huku Baadhi ya wananchi wakiokolewa wakiwa taabani na kupelekwa katika Hospitali ya Manispaa ya Singida.
Wasafi Media tumekita Kambi katika eneo hili ambapo pamoja na Mambo mengine Tumewataarifu Wataalamu wa Nyuki na Jeshi la Zimamoto Juu ya Kadhia hii na Tayari wamefika kutoa Msaada na kuwadhibiti nyuki hao.
Zoezi la Kuwadhibiti Wadudu hao Bado Linaendelea Katika Eneo la Tukio. Endelea kufuatilia kurasa zetu kwenye mitandao ya kijamiii kwa taarifa zaidi
Leave a Reply